Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (REA III) katika kutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mjimwema wilaya ya Mtwara
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amempa miezi mitatu mkandarasi wa mradi wa usambazaji wa Umeme Vijijini (REA III) JV RADI, AGUILA & NJARITA ELECTRICAL SERVICES kuhakikisha anafikisha umeme kwenye vijiji 100 vya mkoa wa Mtwara.
Byakanwa ameyasema hayo novemba 28,2018 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mradi huo ya maendeleo kwenye vijiji vya wilaya ya Mtwara.
Amesema haridhishwi na kasi ya mkandarasi huyo kwani muda aliotumia tangu asaini mkataba haulingani na kazi aliyoifanya kwani makubaliano ya mkataba wa kazi hiyo inatakiwa kukamilika ifikapo Juni, 2019.
“Siwezi kuvumilia huo ulegelege wa kufanya kazi, nataka kazi hii ikamilike kwa wakati, Nakupa miezi mitatu, Kati ya vijiji 167 ulivyokabidhiwa kwa mkoa mzima uwe umekamilisha vijiji 100”. Amesema Byakanwa
Aidha byakanwa amesema tangu mkataba umesainiwa mkandarasi huyo ameshafikisha umeme kwenye vijiji 4 tu vya wilaya ya Mtwara jambo ambalo linatia mashaka iwapo ataweza kumaliza kazi hiyo kwa muda uliobaki.
Kwa upande wake Ahmed Abdallah Hemed amesema maandalizi ya kumalizia mradi huo yanaenda vizuri na kwamba utekelezaji wa mradi umechelewa kutokana na taratibu ndogondogo ikiwemo kuchelewa kupatikana vifaa pamoja na taratibu za kisheria. Pamoja na changamoto hiyo ameahidi kumaliza kazi kwa wakati.
Wakizungumzia uamuzi uliotolewa na mhe. m kuu wa Mkoa wananchi wa kijiji cha Mjimwema kilichoko Wilaya ya Mtwara wameishukuru serikali kwa kufuatilia utekelezaji wa mradi huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.