pongezi kwa JPM
“Bado naendelea kusisitiza vyombo ninavyovisimimia vya Ulinzi na Usalama waendelee kufanya shughuli zao katika maeneo (Mtwara) Kwa sababu tunajua kuna watu ambao tunawatafuta, wamefanya uhalifu katika maeneo yetu, wamekimbilia Msumbiji. Sasa wasije wakatumia fursa hii ya kurudi huku ndani. Lazima tukabe maeneo haya.
Hakuna penati itakayopigwa bila kukabwa. Na anayesimamia chombo chochote kilichoko chini yangu. Ikitokea hawa ambao wanataka kutumia mwanya wa kurudi na baadaye ikabainika ni wahalifu na hawakuwachuja vizuri, basi huyo anayesimamia chombo hicho atapata TAABU SANA. Atapata msukosuko. Iwe ni Jeshi la Polisi. Iwe ni Magereza. Iwe ni Uhamiaji, Zimamoto, Vitambulisho. Watapata TAABU SANA”.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. KANGI LUGOLA. Julai 18. 2018. Mjini Mtwara.
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.