Karibuni Mtwara. Mkoa unaoongoza kwa uzalishaji wa korosho hapa nchini. Ni mji ambao umejizolea umaarufu kwa kuwa na Gesi Asilia ya kutosha kiasi cha kutabiriwa kuwa mhimili wa uchumi wa Tanzania kwa miaka ijayo. Maeneo makubwa ya vivutio vya uwekezaji mkoani Mtwara ni pamoja na
•Kugundulika kwa gesi asilia ambacho ni kichocheo kikubwa cha uwekezaji kutokana na uwezekano wa kuwepo Nishati ya umeme wa kutosha.
•Hifadhi 15 ya misitu iliyotawanyika sehemu mbalimblai hapa Mkoani
•Mtandao wa barabara wa urefu wa kilometa 6149.8 unaounganisha Tanzania na Msumbiji
•Bandari ya Mtwara ambayo ina kina kirefu na upana wa kutosha kiasi cha kuifanya kuwa moja ya bandari bora duniani
•Vivutio vya utalii ikiwemo pwani ya Mnazi.
•Makumbusho ya kale eneo la Mikindani
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.