Serikali ya Tanzania imepokea mkopo wa Shilingi Bilioni 268 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mnivata - Newala hadi Masasi kwa kiwango cha lami kwa urefu wa Kilomita 160.
Barabara ya Mtwara –Newala –Masasi (210km) ni sehemu ya Barabara ya Kusini inayotoka Mtwara hadi Masasi kupitia Tandahimba na Newala. Barabara hiyo imetambuliwa kama ukanda wa kimkakati katika mtandao wa barabara Tanzania. Barabara ya Mtwara-Newala-Masasi inaanzia Magomeni mkoani Mtwara ambayo ni takriban kilomita 5 kutoka katikati ya mji wa Mtwara na kuishia Masasi ambapo inaungana na Barabara ya Mingoyo-Tunduru.
Kwa hatua ya awali barabara hiyo ilijengwa kwa kiwango cha lami kilomita 50 kutoka Mtwara hadi Mnivata, na kubakiza kilomita 160.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkopo huo Dar es salaam leo tarehe 25/11/2021, Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba amesema kujengwa kwa Barabara hiyo kutafungua fursa nyingi za ufanyaji wa biashara kutoka Bandari ya Mtwara kwenda maeneo mengi na Nchi na Mataifa ya jirani na pia kurahisisha shughuli za uchumi ikiwemo utafiti wa gesi ya Mtwara.
Amesema mkopo huo pia utawezesha ujenzi wa Daraja Mwiti lenye urefu wa Kilomita 83 pia kununua magari mawili ya kubebwa wagonjwa katika maeneo ya mradi huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.