Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba amewataka wananchi wa Wilaya ya Tandahimba kujiandaa na uchaguzi wa serikali za Mitaa. wito huo ameutoa wiki hii katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mchichira kata ya Mchichira Tarafa ya Mchichira wilayani hapo.
Amesema uchaguzi wa serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 hivyo wananchi wanapaswa kujiandaa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu ili kuwapata viongozi bora.
“Wananchi hakikisheni mnatumia haki yenu kuchangua viongozi bora. Hawa ndio mtawapa mamlaka ya kuwaongoza katika kujiletea maendeleo” amesema Walyuba
Aidha, Mhe. Waryuba amewaambia wakulima wa korosho ambao bado hawajapata pesa zao kuwa watapatiwa pembejeo kwa asilimia mia moja bila kutoa malipo yoyote na kwamba wakishapatiwa pesa zao ndipo watakapolipa madeni hayo.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu Mheshimiwa Waryuba ameuvunja uongozi wa kikundi Cha wakulima cha Mpunga maji ambacho kimeshindwa kuuendesha mradi wa mashine ya kukoboa mpunga ulioanzishwa na serikali kwa lengo la kuongeza thamani ya zao la mpunga na kuinua kipato cha wakulima.
Amesema viongozi hao wameshindwa kuendana na Kasi ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli kwani wamekuwa wakisababisha migogoro isiyokwisha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.