Mwenyekiti waCCM Mkoa Yusuph Said Nannila akimkabidhi Kadi ya CCM Diwani wa kata ya MakongaMussa Makungwa mara baada ya kutangaza kujitoa CUF na kuhamia CCM
Diwani wa kata ya Makonga wilayani Newala MussaMakungwa amehama kutoka Chama cha Wananchi CUF na kujiunga na Chama chamapinduzi. Uamuzi huo ameufanya wiki hii wakati wa ziara ya Mheshimiwa WaziriMkuu aliyoifanya Wilayani hapo.
Akitangazakukihama chama hicho Makungwa amesema ameamua kufanya hivyo ili kuungana naRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Magufuli katikajitihada za kuwaletea maendeleo watanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha MapinduziMkoa wa Mtwara Yusuf Said Nannila amemshukuru Diwani huyo kwa kufanya uamuzi sahihina kuwataka madiwani wengine kuiga mfano wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.