Jana Julai 27, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa Mikoa, Wizara na Wilaya.
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi na uhamisho huo ili kujaza nafasi zilizo wazi kufuatia baadhi ya viongozi kustaafu, kuteuliwa katika nafasi nyingine na wengine kuachwa.
Miongoni mwa mabadiliko aliyoyafanya ni pamoja na Dkt. Jilly Elibariki Maleko aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara pamoja na Moses Machali aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu.
Uteuzi wenyewe huu hapa.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu RAPHAEL MUHUGA amestaafu.
Wakuu wa Mikoa ambao hawakutajwa katika mabadiliko haya wanaendelea na nyadhifa zao kama kawaida.
Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa kama ifuatavyo:
Makatibu Tawala wa mikoa wafuatao wamehamishwa vituo vyao vya kazi.
Aidha, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu kwa baadhi ya Wizara kama ifuatavyo;
Halikadhalika Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya na wengine kuhamishwa vituo vya kazi kama ifuatavyo;
Tarehe ya kuapishwa kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa itatangazwa baadaye.
Wakuu wa Wilaya wataapishwa na Wakuu wao wa Mikoa kwa utaratibu utakaopangwa na Mikoa husika.
BREAKING: JPM ATANGAZA MABADILIKO WAKUU WA MIKOA/WILAYA… JOKATE, JERRY MURO WAULA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.