• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

FCT YAAHIDI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADAU KATIKA KUKUZA USHINDANI WA HAKI NA KUMLINDA MLAJI

Posted on: May 3rd, 2024



FCT yaahidi kuendelea kutoa  ushirikiano kwa wadau katika kukuza ushindani wa haki na kumlinda mlaji


Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Bahati Geuzye, amesema Baraza la Ushindani (FCT) litaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli za kiuchumi katika masuala ya kiushindani na udhibiti wa Soko.

Ameyasema hayo Mei 3, 2024 Mkoani humo wakati  akifungua  semina ya elimu  kwa wadau iliyoandaliwa FCT kwa Lengo la kutoa elimu kwa wadau kuhusu haki na wajibu wao ili kustawisha ushindani wa haki na kumlinda mlaji katika soko.

Akiwahutubia wadau hao wakiwemo wawekezaji, watoa huduma, wafanyabiashara, na walaji/watumiaji na Taasisi  za umma, 

Geuzye amesema kuwa semina hii itasaidia wadau kuongeza kasi ya uwajibikaji katika soko na kutambua namna bora ya kutatua changamoto na migogoro ya kiushindani.

Naye Mkuu wa Idara ya Uchumi FCT, Bw. Kulwa Msogoti, ameongeza kuwa Baraza linahamasisha wadau wote wafanyabiashara, wawekezaji, watoa huduma, na walaji wawasilishe mashauri yao FCT iwapo hawajaridhika na maamuzi yanayotolewa na Tume ya Ushindani na Mamlaka za udhibiti kama vile EWURA, LATRA, PURA, TCAA, na TCRA.

Vilevile Afisa Sheria Mkuu wa FCT, Bi. Hasfa Said, amesisitiza kuwa FCT inatekeleza Sheria ya Ushindani ya Bunge na Kanuni za Baraza la Ushindani za mwaka 2012 na linaweza kutoa adhabu kwa wale wanaokiuka sheria hii, ikijumuisha faini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Chemba of Commerce Mkoa wa Mtwara, Bw Juma Napinda, amesema  semina ya FCT imeleta mwamko wa wadau mbalimbali kujua wapi wanaweza kupata haki zao iwapo mlalamikaji anahisi hajatendewa haki, anaweza kukata rufaa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC),  Bi Mwajuma Ankoni, amesema semina hii imewapa mwanga na elimu watakayoitumia siku za mbeleni na watakuwa mabalozi kwa wafanyabiashara ndani ya mkoa na nje ya mkoa.

Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Matakatifu Agotino (SAUT) Mtwara, Bw. Elia Charles, amesema semina hii ina manufaa na inampa uhalisia wa masuala ya biashara unaomsaidia kufundisha wanafunzi na itasaidia wafanyabiashara  kuelewa namna ya ubora wa ushindani katikakufanya biashara  bila kuathiri  mlaji.

Naye Msindikija wa Vyakula Mbalimbali vya Asili, Bi Zainabu Abdallah, amesema semina hii itawasaidia wafanyabiashara kupata elimu kuhusu mahali pa kukata rufaa iwapo hawakubaliani na hukumu.


Mei 3, 2024.


#TunaifunguaMtwara

#KaziIendelee


Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU KARIBU MTWARA

    May 17, 2025
  • JESHI LA POLISI TANZANIA YATUPIA JICHO MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MTWARA

    May 20, 2025
  • MWENGE WA UHURU MASASI

    May 18, 2025
  • NANYUMBU WAANZISHA BIO ZA MWENGE MTWARA

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.