TANESCO
KAMATI YA PIC YAFURAHISHWA NA UFUNGAJI WA MTAMBO WA UMEME MTWARA.
Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) imelipongeza shirika la umeme Tanzania –TANESCO kwakutelekeza mradi wa ufungaji wa mtambo mpya wa kuzalisha umeme megawati 20 ndani ya miezi mitatu.
Akizungumza wakati wa ziara ya kama hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya (PIC) Deus Sangu amesema kuwa mtambo huo unaenda kuondoa tatizo la umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Amesema kuwa mradi huo unauwezo wa kuzalisha megawati 20 ikiwa ni utelekezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu alipofanya ziara yake Septemba mwaka jana.
“Mikoa hii ilikuwa na changamoto kubwa ya umeme mtambo huu umesimikwa na kampuni ya kizalendo ambayo imefanyakazi nzuri na kwa wakati ni vema wakandarasi wengine wakaiga uzalendo huu Mradi huu unaenda kuleta mapinduzi makubwa”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-hanga amesema kuwa huu mtambo wa utazalisha umeme megawati 20 ambao umekuja kuongeza nguvu ya uzalishaji wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
“Mradi huu umeshaanza kuzalisha umeme ambapo unaenda kuongeza megawati 20 na kituo cha zamani kinazalisha megati 21 ambapo kwa sasa zitakuwa megawati 41 hivyo kuleta ufanisi zaidi”
“Mtambo huu ni suluhu ya muda mfupi ambapo ipo suluhu ya muda mrefu ya kuleta mradi mkubwa wa umeme wa grid ya taifa ambapo hadi kufikia 2026 Mtwara itakuwa imeunganishwa kwenye grid ya taifa ambapo mitambo hii itabakia kuwa miradi ya dharula”
“Kuanzia mwezi huu tatizo la kukatika umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara litakuwa limeisha ambapo huduma ya umeme itakuwepo bila kuwa na changamoto yoyote” amesema Nyamo-hanga.
Machi 25, 2024
#TunaifunguaMtwara
#KaziIendelee
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.