Kongamano na Jukwa la Ushirika Mkoa wa Mtwara limeanza kufanyika katika Viwanja na Ukumbi wa Shule ya SEKONDARI , Mtwara Sisters ( PARISH ). Mgeni Rasmi alitarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Brigedia General Marco Elisha Gaguti ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Dustan Kyobya. Kongamano hili litafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia leo tarehe 16-17/06/2021 ambapo Naibu katibu mkuu Wizara ya Kilimo Prof. Siza Tumbo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwa siku ya pili ya tarehe 17/06/2021.
Kongamano limewakutanisha Wakulima, wanachama na viongozi wa vyama vya Ushirika wote wa Mkoa wa Mtwara. Katika kongamano hilo kutakuwa na mafunzo mbalimbali ikiwemo namna Bora ya kuimarisha Ushirika, kuongeza uzalishaji, uongezaji wa thamani mazao, maonesho ya bidhaa na huduma za wanaushirika, mapambano dhidi ya Rushwa, mchango wa ushirika katika kuelekea Tanzania ya Viwanda n.k.
Aidha kongamano hili limehudhuriwa pia na Wakuu wa Wilaya, Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa, Makatibu Tawala Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi, Maafisa Kilimo na Ushirika,Viongozi wa Dini, Wakuu wa Taasisi na Wawakilishi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ( MoCU).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.