• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

Maafisa Utumishi watakiwa kubuni mipango ya motisha kwa watumishi

Posted on: November 20th, 2017

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akizungumza na wajumbe wa Warsha (hawapo pichani)


Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Alfred Luanda amewataka Maafisa Utumishi kubuni njia nzuri itakayotoa motisha kwa watumishi ili kuwafanya wawe na moyo wa kufanya kazi ndani ya mkoa. Amesema anatambua ugumu wa mazingira na huduma katika baadhi ya maeneo ndani ya mkoa lakini mipango mizuri yenye kutoa motisha kwa watumishi itawafanya watumishi waendelee kuwa na moyo wa kufanya kazi katika maeneo waliyopangiwa.

Luanda ameyasema hayo leo wakati akifungua Warsha ya kuandaa mipango ya motisha ya watumishi wa serikali za mitaa iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maafisa Tabibu Mtwara (COTC) ikiwahusisha Maafisa wa idara mbalimbali za halmashauri wakiwemo Maafisa Utumishi.

Katika warsha hiyo iliyoandaliwa na shirika la Watu wa Marekani (USAID) kupitia mradi wake wa PS3 amesema jambo kubwa ni halmashauri zenyewe kujiangalia ili yale ambayo wanauwezo nayo yapewe kipaumbele katika utekelezaji.

‘Ni kweli kuwa utekelezaji wa baadhi ya mambo unahitaji fedha nyingi mfano, ujenzi wa barabara, ujenzi wa nyumba za watumishi, miundombinu ya mawasiliano na mengine mengi. Haya Serikali itaendelea kuyashughulikia kwa kadiri inavyopata uwezo wa kutekeleza’.

Amesisitiza kuwa utoaji wa motisha kwa watumishi utakuwa na maana tu kama utakuwa endelevu hivyo ni vema mipango ikajengwa ndani ya mifumo ya utendaji wa Halmashauri, ili iwe rasmi, endelevu na kuingizwa katika mifumo ya ufuatiliaji na uwajibikaji.

Kwa upande wake Msimamizi idara ya Rasilimali Watu Kanda ya Kusini, Mradi wa PS3, Restituta Evaristy Masau amesema wazo la motisha kwa watumishi wa serikali za mitaa limekuja kufuatia utafiti uliofanywa na shirika lao wakipitia sera ya motisha kwa wafanyakazi na kubaini kuwa ni ngumu kuitekeleza.

Kufuatia utafiti huo ndipo shirika likaona umuhimu wa kuwapa mafunzo Maafisa wa Halmashauri ili waweze kuandaa mpango unaotekelezeka. Anasema mradi huo wa PS3 unaodhaminiwa na watu wa marekani una nia ya kuhakikisha watanzania wanaondokana na changamoto wanazokutana nazo katika mazingira ya kazi, hivyo kuachana na tabia ya kuhama hama kituo kimoja kwenda kingine kwa kisingizio cha mazingira magumu ya kazi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Warsha, Tamko Mohamed Alli ambaye pia ni Afisa Utumishi Manispaa ya Mtwara Mikindani anasema ziko changamoto nyingi katika halmashauri za mkoa wa Mtwara ambazo zinawafanya watumishi kupenda kufanya kazi eneo moja na kuchukia maeneo mengine. Anasema kubwa linalowavutia ni miundombinu ya eneo husika hivyo warsha hiyo itakayoendeshwa kwa siku tano itasaidia kwa kiasi kikubwa kupata mpango mpya wa motosisha kwa wafanyakazi.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU KARIBU MTWARA

    May 17, 2025
  • JESHI LA POLISI TANZANIA YATUPIA JICHO MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MTWARA

    May 20, 2025
  • MWENGE WA UHURU MASASI

    May 18, 2025
  • NANYUMBU WAANZISHA BIO ZA MWENGE MTWARA

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.