RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli amewahakikishia na kuwatoa hofu wakulima wa zao la korosho wakiwemo ambao korosho zao zilikuwa zimeshikiliwa kwa tuhuma ya kununua kinyume na utaratibu maarufu kama kangomba kuwa watalipwa fedha zao.
Hayo yamesemwa leo na na Mhe. Magufuli wakati wa uzinduzi na uwekaji na jiwe la msingi la upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara uzinduzi ambao umefanyika katika viwanja hivyo.’
Amesisitiza kuwa msamaha huu hautaendelea hivyo wafanyabiashara hao wasirudie tena .
Aidha, Rais Magufuli ametoa ufafanuzi wa uamuzi wa serikali kununua korosho hizo baada ya kuona wanunuzi wanataka kununua kwa bei ya chini kitendo ambacho kingewanyonya wakulima.
“Kunuuna korosho kwa bei ya chini ni kuwanyonya wanyonge kwa hiyo serikali ikaona ipo haja ya kununua korosho hizo ili kuwasaidia wakulima kupata haki zao vizuri”,Amesema DK. Magufuli
Hata hivyo ametoa agizo kwa viongozi katika mikoa yote inayolima zao hilo kuhakikisha wanasimamia zao hilo ili kumsaidia wakulima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.