• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ashiriki misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa iliofanyika Kijiji cha Lupaso Wilaya ya Masasi

Posted on: July 24th, 2021

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 24, 2021 ameshiriki misa ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Rais wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa iliofanyika  Kijiji cha Lupaso Wilaya ya Masasi. Akizungumza baada ya misa hiyo, Makamu wa Rais amesema mchango wa hayati Benjamin Mkapa kwenye mageuzi ya kiuchumi; mapambano dhidi ya rushwa ambayo yalipelekea watanzania kumpa jina la “Bwana Msafi”; mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi; kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa Umma; na usuluhishi wa migogoro ya kisiasa katika nchi za DRC, Burundi, Kenya kamwe hautafutika.  

 Makamu wa Rais amesema viongozi wanajifunza kutoka kwa Hayati Benjamin William Mkapa ujasiri na uthubutu wake katika kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya Taifa. Aidha amesema hayati Mkapa ameacha alama ya   umuhimu wa kuwajibika na kusimamia misingi ya haki na usawa katika kuwahudumia wananchi wote. Aidha Makamu wa Rais amesema Hayati Benjamin William Mkapa alitambua kwamba Utegemezi una hatari nyingi na hivyo ni lazima kujizatiti kujitegemea kama nchi. Alisema hatima ya Tanzania na Afrika iko mikononi mwa watanzania na Waafrika wenyewe.  Na alihimiza muda wote kwamba wajibu wa kwanza ni kutatua matatizo ya nchi yetu na ya bara letu la Afrika wenyewe iwe ni matatizo ya kijamii, kisiasa au kiuchumi ili kukuza ustawi wa Taifa na bara zima.

   Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais amewataka wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Korona ambao umeingia katika wimbi la tatu lililo hatari Zaidi. Amewasihi viongozi wa dini pamoja na waumini wa dini zote kumwomba Mungu msamaha ili afukuze ugonjwa huu duniani ili watu wake wamtukuze na kumwabudu kwa furaha na amani bila hofu ya KORONA.  Aidha amewaomba viongozi wa dini na watanzania wote kuendelea kuiombea nchi amani na kuwaombea viongozi wa Serikali hekima itokayo kwa Mungu mwenyezi ili kuongoza taifa kwa ufanisi.

 Akitoa mahubiri katika misa hiyo, Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo amesema watanzania wanatakiwa kuendelea kumuombea Hayati Benjamin Mkapa na kuyaenzi yale yote mema alioyafanya akiwa duniani. Kwa upande wake msemaji wa familia ya Hayati Benjamin Mkapa bwana William Urio amesema Hayati Mkapa aliilinda imani ya dini yake wakati wote wa Maisha yake na kumtanguliza Mungu katika shughuli zake zote.

 Aidha ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaunga mkono katika kufanikisha shughuli ya kumaliza msiba wa Hayati Benjamin Mkapa. Misa hiyo imehudhuriwa pia na mjane wa Hayati Benjamin Mkapa , mama Anna Mkapa,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula, Mkuu wa Mkoa Mtwara Brig. Jenerali Marco Gaguti pamoja na viongozi mbalimbali. Baada ya Misa hiyo, Makamu wa Rais alipanda mti katika eneo iliopo nyumba ya Hayati Benjamin William Mkapa.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • CRDB KANDA YA KUSINI YAISHIKA MKONO MTWARA MAANDALIZI YA UMISETA TAIFA

    May 27, 2025
  • KUELEKEA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, MIKOKO 6,000 YAPANDWA MTWARA.

    May 31, 2025
  • KAMATI YA LISHE MKOA WA MTWARA YAKUTANA

    May 30, 2025
  • MIRADI YA UJENZI ITOE AJIRA KWA WANANCHI” WAZIRI ULEGA

    May 27, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.