Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akikagua nyaraka za ujenzi wa Hospitali ya halmashauri
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ameagiza jeshi la polisi kumshikiria mhandisi wa halmashauri ya wilaya ya Masasi Edward Msafiri kwa kushindwa kusimamia ipasavyo na kusababisha dosari za ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya wilaya hiyo na kituo cha afya cha kata ya Chiungutwa.
Ujenzi wa hospitali hiyo na kituo cha afya unaotumia fedha kutoka serikali kuu ulipaswa kukamilika Julai 30 mwaka huu lakini miradi yote miwili inatekelezwa kwa kusuasua.
Akiwa ameambatana na wataalamu wa Sekrtarieti ya Mkoa Mhe. Mkuu wa Mkoa alisikitishwa na mwennendo wa Ujenzi huo. Amesema hii ni mara ya pili anatembelea na kutoa maagizo ambayo alitegemea yangekuwa yametekelzwa.
AIdha amemuagiza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha wanamsimamia mjenzi huyo.
Kama nikirudi amra ya pili na kukuta shughuli bado inasuasua, nitapanda juu zaidi. (Akimaanisha kuwachukulia hatua wasimamizi wakuu)
Hospitali ya wilaya ya Masasi ni kati ya hospitali mpya zinazojengwa halmashauri mbalimbali hapa nchini kwa kutumia fedha kutoka serikali kuu ikiwa ni mikakati ya serikali ya awamu ya tano kuboresha huduma za afya kwa kosogeza huduma hizo karibu na wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.