• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

MKandarasi wa REA Mtwara apewa miezi 3

Posted on: November 29th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini (REA III) katika kutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mjimwema wilaya ya Mtwara

 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amempa miezi mitatu mkandarasi wa mradi wa usambazaji wa Umeme Vijijini (REA III) JV RADI, AGUILA & NJARITA ELECTRICAL  SERVICES kuhakikisha anafikisha umeme kwenye vijiji 100 vya mkoa wa Mtwara.

Byakanwa ameyasema hayo novemba 28,2018 wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mradi huo ya maendeleo kwenye vijiji vya wilaya ya Mtwara.

Amesema haridhishwi na kasi ya mkandarasi huyo kwani muda aliotumia tangu asaini mkataba haulingani na kazi aliyoifanya kwani makubaliano ya mkataba wa kazi hiyo inatakiwa kukamilika ifikapo Juni, 2019.

“Siwezi kuvumilia huo ulegelege wa kufanya kazi, nataka kazi hii ikamilike kwa wakati, Nakupa miezi mitatu, Kati ya vijiji 167 ulivyokabidhiwa kwa mkoa mzima uwe umekamilisha vijiji 100”. Amesema Byakanwa

Aidha byakanwa amesema tangu mkataba umesainiwa mkandarasi huyo ameshafikisha umeme kwenye vijiji 4 tu vya wilaya ya Mtwara jambo ambalo linatia mashaka iwapo ataweza kumaliza kazi hiyo kwa muda uliobaki.

Kwa upande wake Ahmed Abdallah Hemed amesema maandalizi ya kumalizia mradi huo yanaenda vizuri na kwamba utekelezaji wa mradi umechelewa kutokana na taratibu ndogondogo ikiwemo kuchelewa kupatikana vifaa pamoja na taratibu za kisheria. Pamoja na changamoto hiyo ameahidi kumaliza kazi kwa wakati.

Wakizungumzia uamuzi uliotolewa na mhe. m kuu wa Mkoa wananchi wa kijiji cha Mjimwema kilichoko Wilaya ya Mtwara wameishukuru serikali kwa kufuatilia utekelezaji wa mradi huo.



Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU KARIBU MTWARA

    May 17, 2025
  • JESHI LA POLISI TANZANIA YATUPIA JICHO MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MTWARA

    May 20, 2025
  • MWENGE WA UHURU MASASI

    May 18, 2025
  • NANYUMBU WAANZISHA BIO ZA MWENGE MTWARA

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.