Nyumba za watumishii wa Zahanati ya Imekuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara zilizojengwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa.
Taasisi ya Benjamini Mkapa imejenga jumla ya nyumba 50 za watumishi wa Afya mkoani Mtwara. nyumba hizo zimejengwa katika zahanati na vituo vya afya sehemu mbalimbali mkoani hapa huku zikigharimu taribani milioni 53 hadi 68 kila nyumba.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa nyumba hizo zilizojengwa kati ya mwaka 2011 na 2015 Mtendaji Mkuu wa Benjamini Mkapa Foundation Dkt. Ellen Mkondya Senkoro amesema waliamua kufanya hivyo kutokana na mahitaji makubwa ya nchi na wamejenga jumla ya nyumba 480 nchi nzima.
Amesema ujenzi huo ulizingatia vituo ambavyo vilikuwa havifanyai kazi kutokana na changamoto ya nyumba za watumishi na hivyo kuwezesha kufanya kazi na kusaidia kwa kiasi kikubwa huduma kwa jamii.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kawawa, Hadija Marekana pamoja Joseph Sheduo wa zahanati ya Imekuwa kwa nyakati tofauti wameshukuru taasisi hiyo kwa msaada huo na kwamba imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo la huduma ya afya kwa jamii.
Wamesema kabla ya ujenzi wa nyumba katika zahanati hizo walikuwa wakilazimika kusafiri kutoka vijiji jirani kwenye makazi yao jambo ambalo lilikuwa likikwamisha huduma za haraka hasa nyakati za usiku.
Kwa upande wake Fatuma Selemani wa kijiji cha Imekuwa anasema wamepata ahueni kubwa baada ya ujenzi wa nyumba hizo kwani hata usiku wa manane wanawaamusha waganga na kupata huduma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.