• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

DC Moses Machali akabidhiwa kinyago cha huzuni

Posted on: December 29th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa akikabidhi kinyago cha huzuni uongozi wa Wilaya ya Nanyumbu


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amekabidhi kinyago cha huzuni kwa viongozi wa wilaya ya Nanyumbu kufuatia kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa kwa darasa la saba  mwaka 2018.

 Kinyago hiki chenye lengo la kuhamasisha ushindani wa kielimu kwa halmashauri za mkoa wa Mtwara kwa ngazi zote kimetolewa mbele ya wajumbe wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mtwara katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mtwara Disemba 28, 2018.

Awali wakijadili mbinu za kuhamasisha ushindani wa kimasomo kwa wanafunzi wa ngazi zote ndani ya mkoa wajumbe walikubaliana kuweka utaratibu wa kuzungusha kinyago hicho kinachomuonesha baba na mama wakiwa katika simanzi na majonzi makubwa.

 Mheshimiwa Byakanwa amesema licha ya Nanyumbu kupokea kinyago bado wanajukumu la kuongoza kikao cha wadau wa elimu mkoa kitakachofanyika mapema mwaka 2019  ambapo pamoja na mambo mengine watatakiwa kuwaambia wajumbe ni kwa nini wamekuwa wa mwisho na mikakati gani waliyo nayo kujitoa katika nafasi hiyo.

Akizungumza baada ya kupokea kinyago hicho, Mbunge wa jimbo la Nanyumbu Mheshimiwa Dua William Nkurua amesema wamepokea kinyago hicho kwa mikono miwili na kwamba kitawasidia kujitafakari na kuongeza juhudi ili kujitoa katika aibu hiyo.

Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo Mheshimiwa Moses Joseph Machali amesema wanaenda kujipanga ili kuhakikisha kinyago hicho kinakabidhiwa wilaya nyingine mwaka ujao. Amesema zipo changamoto nyingi ambazo wamezianisha ikiwemo upungufu wa walimu, utendaji kazi usioridhisha pamoja na miundombinu mibovu.

“Tutahakikisha changamoto zote tunazitatua ili mwakani kinyago hiki kichukuliwe na wilaya nyingine”. Amesema Machali

Kwa upande wake mwakilishi wa gazeti la Habari leo Mkoa wa Mtwara Sijawa Omary amepongeza maamuzi ya kikao hicho ya kuizawadia kinyago halmashauri iliyoshika nafasi ya mwisho kwa ufaulu kwenye mitihani ya darasa la saba.

“Uamuzi huo ni mzuri kwani unahamasisha ushindani. Wanachotakiwa kufanya sasa ni kukipa jina ambalo litakuwa na mtazamo wa mkoa wa Mtwara. jina ambalo litawafanya wamiliki wake kuhuzunika kweli” Amesema Sijawa.

Tangu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa huu mapema mwaka huu ameahidi kuhakikisha elimu ya mkoa wa Mtwara inainuka ambapo mafaniko yake yameanza kuonekana.

Mwaka 2018 mkoa umekuwa katika nafasi ya nane kitaifa kutoka nafasi ya 22 katika matokeo ya darasa la Saba mwaka 2017 huku ukishika nafasi ya kwanza katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018.


video yake hii HAPA


Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU KARIBU MTWARA

    May 17, 2025
  • JESHI LA POLISI TANZANIA YATUPIA JICHO MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MTWARA

    May 20, 2025
  • MWENGE WA UHURU MASASI

    May 18, 2025
  • NANYUMBU WAANZISHA BIO ZA MWENGE MTWARA

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.