Kutokana na umuhimu na manufaa ya matumizi ya gesi asilia katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira, Waziri wa Nishati Dkt. Merdard Kalemani ameliagiza shirika la maendeleo ya Petrol nchini (TPDC) kuongeza kasi ya usambazaji wa nishati ya gesi majumbani ili kupunguza athari za kimazingira zinazotokana na matumizi mengine ya nishati.
Kalemani ametoa maagizo hayo leo mkoani Mtwara kwenye hafla ya uzinduzi wa awamu ya pili ya mradi wa usambazaji gesi asilia majumbani.
Amesema uhitaji wa gesi asilia ni mkubwa hivyo shirika linapaswa kuongeza kasi ya kusambaza nishati hiyo muhimu na salama.
Akizungumzia hatua ya uzinduzi wa awamu ya pili ya matumizi ya gesi asilia amesema serikali imetumia zaidi ya Milion 960 kujenga miundombinu ya gesi katika nyumba 300 zilizofikiwa na mradi .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.