Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Mathew Kundo leo tarehe 04/10/2024 ameanza ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji ikiwemo ile ya moboresho ya miundo mbinu pamoja na uchimbaji wa visima.Mhandisi Kundo pia amekagua vyanzo vya maji vya Mnyawi na Makonde ambavyo vitaenda kutatua changamoto ya maji Nanyamba mji, wilaya ya Tandahimba na wilaya ya Newala.“Serikali ina nia ya kumtua mama ndoo kichwani ndio maana inafanya jitihada zote hizi, Mhe. Rais Samia ametoa zawadi kwa wabunge ambapo kila jimbo litachimbiwa visima vitano.” Alieleza Mhe. Kundo
Katika hatua nyingine Mhe. Kundo amemtaka mkandarasi anaechimba visima vya maji eneo la Maparawe, wilaya ya Masasi kukalimisha kazi hiyo ifikapo tarehe 20/10/2024.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.