Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akifungua kikao cha Mwongozo wa uwekezaji leo Februali 10, 2019
Mkoa wa Mtwara unajipanga kuhakikisha unaandaa mwongozo wa uwekezaji ambao utawezesha kutangazwa kwa fursa zote za uwekezaji ndani ya Mkoa. Katika kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Boma Mkoa ulioko Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wajumbe kwa pamoja wameridhia mpango huo ulenge kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji huku dunia nzima ikijulishwa jinsi gani wanaweza kunufaika na mazingira hayo.
Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amesema Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) wameridhia kufadhili uandaaji wa mpango huo ambapo Taasisi ya ESRF imepewa kazi hiyo. Amesema ili kuhakikisha lengo la mkoa linafikiwa ni lazima wadau wote kujiandaa ili kutoa ushirikiano kwa waandaaji.
Wakichangia mawazo wajumbe wa kikao hicho waesema Mkoa unazo fursa nyingi zinazoweza kusaidia katika kuhamasisha uwekezaji. fursa hizo ni pamoja na miundombinu ya usafiri ikiwemo barabara, uwanja wa Ndege, bandari pamoja na ardhi nzuri yenye rutuba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.