Sijawa Omary, Mtwara
MKUU wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ametoa wiki tatu kwa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani hapa kuhakikisha wanatenga viwanja maalumu kwa ajili ya ujenzi wa viwanda hasa nchi inapoelekea katika uchumi wa viwanda.
Mhe. Byakanwa amebainisha hayo wakati wa kikoa na madiwani pamoja na watumishi wa halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye halmashauri hiyo.
Alisema kuwa, viwanja vyote vilivyopo kwenye halmashauri hiyo ambavyo vimetelekezwa na wamiliki kwa muda mrefu bila kufanyiwa mazingira ya usafi au huduma yeyote vichukuliwe kutokana na wamiliki wake kushindwa kumiliki rasilimali hiyo.
“Viwanja vingapi kama halmashauri mumetenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda? Nashangaa kuona tunaelekea katika uchumi wa viwanda na hakuna viwanja vya kutosha ambayo vimetengwa maalumu kwa ajili hiyo”, Alisema Byakanwa
Panapotekea fursa hizo ni vema kufanya maandalizi mapema ili kuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza hapo baadae katika rasilimali hiyo.
Sanjali na hilo mkuu huyo amezitaka halmashauri zote mkoani hapa kuhakikisha zinasimamia ipasavyo pesa zote za miradi ya maendeleo ili kufikia malengo yanayokusudiwa katika mkoa huo.
“Nataka kuona halmashauri zote zinasimamia vema miradi yote ya maendeleo kwenye halmashauri zetu kikubwa tuweze kufikia lengo tunalokusudia”,Alisema Byakanwa
Kaimu Mkurugenzi katika halmashauri hiyo, Tamko Ally alisema yale yote yaliyoangizwa na Mkuu huyo kama halmashauri yatafanyiwa kazi kwa vitendo ili kufikia malengo husika.
Katika swala la kutenga na kuangalia viwanja ambavyo wamiliki wameshindwa kuvihudumia pia litafanyiwa kazi kwa umakini wake hasa nchi inapoelekea katika uchumi huo wa viwanda.
Mwisho.
Cpn 1 na 2: Pichani ni mkuu wa mkoa wa mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa hivi karibuni akizungumza na watumishi pamoja na madiwani katika halmashauri ya manispaa ya mtwara mikindani mkaoni hapa katika viwanja vya halmashauri hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.