• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

MTWARA WAPONGEZWA KWA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI

Posted on: October 6th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema serikali imewekeza zaidi ya shilingi milioni mia Tano katika miradi mbalimbali katika mwaka wa fedha wa 2024/25 ambazo zimesaidia kuboresha mfumo wa utoaji huduma katika maeneo mbalimbali.


Akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa vyumba vya madasa katika shule ya msingi Tandika, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Stergomena Tax, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuwaondolea adha wakazi wa Mtwara katika sekta za afya, elimu, kilimo na maji na hivyo kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada hizo  Ili ziweze kuwaletea Maendeleo.


Aidha Kanali Sawala amemweleza Waziri Tax kuwa hivi karibuni serikali Kwa kutambua umuhimu wa wakulima wa korosho katika ukanda wa Kusini  imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 740 kwenye mradi wa makasha ya kupokelea korosho katika msimu mpya wa korosho wa 2024/35 na zaidi ya shilingi bilioni 268 zimewekezwa katika mradi wa barabara ya uchumi ya Mvnivata hadi Masasi  huku zaidi ya shilingi bilioni 300 zikiwekezwa kwenye miradi ya Maji.


Kwa upande wake waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Stergomena Tax  amewashukuru wakazi wa Mtwara Kwa kujitolea Kwa hali na mali kufanikisha Miradi ya Maendeleo.

Akizindua Mradi wa zahanati ya Magomeni iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 100 Mhe Tax amesema dhamira ya serikali ya awamu ya sita ni kuona Kila mwananchi anapata huduma zote za kijamii Kwa wakati na Kwa gharama nafuu.


'' Ndugu wananchi na viongozi mliofika kushuhudia tukio hili kwanza naomba niwafikishie salamu za Mhe Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan, binafsi anasema serikali inatambua changamoto zenu na itaendelea kuzitatua kadri mipango yake na uwezo wa kifedha utakavyoruhusu'' alisisitiza Waziri Tax.

Akiwa katika halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mhe Tax amezindua mradi wa vyumba vya madarasa vilivyo gharimu  shilingi milioni 560 ambapo amesema serikali itahakikisha inatatua  kero zote zinazowakabili  wananchi katika sekta za elimu, afya, maji, barabara na nishati na kuwataka kuitunza miradi hiyo Ili iweze kudumu Kwa  muda mrefu.


''Ndugu wanamtwara Kwa kipindi cha miaka mitatu serikali ya awamu ya sita imewalelea zaidi ya shilingi bilioni 700 ambazo zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo, Kwa ujumla hii ni ishara tosha inayodhihirisha upendo wa hali ya juu kutoka Kwa Rais wetu" alisisitiza Waziri Stergomena Tax.


Aidha Mhe Tax amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo ilikotekelezwa mirada hiyo ya maendeleo kuwa mabalozi wazurii wanaojivunia miradi hiyo na kuisemea vizuri Ili iwe mfano wa kuigwa katika maeneo mengine.


"Kwa hatua ya maendeleo mliyoifikia Mtwara nawaomba mtembee kifua mbele, waambieni wawekezaji njooni umeme upo wa uhakika, maji yapo pia miundombinu ya usafirishaji ni ya uhakika" aliongeza  Mhe Tax.


Kuhusu sekta ya Maji Waziri Tax amesema serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa ya kumtua mama ndoo kichwani ambapo Mkoa wa Mtwara Kwa Miaka mitatu mfululizo umepokea mabilioni ya fedha kutekeleza miradi mbalimbali.

"Jamani nikianza kuyaongelea mafanikio tuliyoyapata kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo tutakesha, Kwa ujumla itoshe kusema Rais wetu Dkt  Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa na anastahili kupongezwa" alisisitiza. Waziri Tax.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ameitumia fursa hiyo  kumshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuuletea Mkoa wa Mtwara miradi ya mabilioni ya fedha katika sekta za elimu, Kilimo na afya hatua ambayo amesema ni kielelezo cha jitihada za serikali katika kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kijamii.


Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SAWALA AAGIZA VYAMA VYA USHIRIKA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WAKULIMA.

    June 24, 2025
  • MKURUGENZI MPYA NANYAMBA NA DAS MPYA MTWARA WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO

    June 23, 2025
  • MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YATAKIWA KUPUNGUZA UTEGEMEZI KWA WAFADHILI.

    June 28, 2025
  • MAREKANI KUTUMIA BANDARI YA MTWARA KUSAFIRISHA BIDHAA

    June 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.