Mtwara Yang’ara Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa Mkoani Ruvuma, Yapata Tuzo na Shilingi Milioni Moja.
Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa lililotamatika Septemba 23,2024 limeinga’arisha nyota ya Mkoa wa Mtwara ambapo Mkoa wa Mtwara umeibuka mshindi wa kwanza katika tasnia ya ngoma za asili kupitia kazi nzuri ya kikundi cha Sanaa cha Mundu.
Katika hotuba yake wakati wa kukabidhi tuzo hiyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema tamasha hilo ni kielelezo cha namna serikali inavyothamini tamaduni zake na kwamba itaendelea kuzienzi na kuzilinda.
Katika shamrashamra za kupokea tuzo hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia alikuwa kiongozi wa msafara amekipongeaza kikundi cha Mundu kwa kuuwakilisha vema Mkoa katika tamasha hilo na kuahidi kuwa Mkoa utaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kukuza utamaduni ikiwemo kuviwezesha na kuviendeleza vikundi mbalimbali vya Sanaa na utamaduni.
Kwa upande wake mwakilishi wa mkoa ambaye alikabidhiwa tuzo hiyo na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Bi Fatuma Mtanda amemshukuru Rais kwa jitihada zake za kuisimamia tasnia ya Sanaa na utamaduni huku akiahidi kuwa kitengo cha Sanaa chini ya idara ya elimu Mkoa kimejipanga kufanya mapinduzi makubwa katika kukuza na kuendeleza utamaduni ikiwemo ngoma za asili.
Naye kiongozi wa kikundi cha Mundu Bw. Said Sandali Chande ameushukuru uongozi wa Mkoa kwa kukilea vizuri kikundi hicho na kusema kuwa tuzo hiyo imeujengea heshima mkoa halikadhalika imewaongezea morali wanakikundi ambao kwa sasa waamini hakuna linaloshindikana.
Katika Tamasha hilo Mkoa wa Mtwara umekabidhiwa tuzo ya mshindi wa kwanza katika ngoma asili pamoja pesa taslimu shilingi 1,000, 000/=
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.