Naibu waziri wa Kilimo Mhe. Omari Mgumba amewatoa mashaka wawekezaji katika sekta ya korosho hapa nchini kwamba Tanzania imeandaa mazingira mazuri ya uwekezaji katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda hususani zao la korosho.
Akizungumza leo katika kongamano la kimataifa la uwekezaji katika sekta ya korosho lililofanyika ukumbi wa Benki Kuu tawi la Mtwara amesema vipo viwanda zaidi ya kumi ambavyo vimekuwepo tangu serikali ya awamu ya kwanza ambavyo teknolojia yake imepitwa na wakati na vingine havifanyi kazi kabisa.
“Nakumbuka mwalimu Nyerere mwaka 1978 hadi mwaka 1980 alijenga viwanda zaidi ya 12 ambavyo kwa sasa teknolojia yake imepitwa na wakati. Baadhi vimekufa na vilivyobaki vimepunguza uzalishaji. Ndiyo maana tumaeamua kuwaita wawekezaji ili kuviendeleza na kuanzisha vingine ili kuongeza uzalishaji”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Geofrey Mwambe amesema wameamua kuandaa kongamoano hilo ili kushawishi wawekezaji wazawa na wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani ili wawekeze katika viwanda vya kubangua korosho katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Pwani kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Tulitarajia kupata wageni mia moja mpaka mia moja hamsini lakini tumepata wawekezaji zaidi ya mia tatu. Kwa idadi hii tumevuka lengo la kongamano letu na tunaimani watakuwa tayari kuwekeza kwenye viwanda vikiwemo viwanda vya korosho. Nashukuru Wakuu wa Mikoa walioshiriki wote wametenga maeneo ya uwekezaji jambo ambalo linarahisisha KAZI”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.