Wajumbe wa Maandalizi ya Maonesho ya Nanenae Kitaifa 2017 wakifuatilia mijadala wakati wa kikao kilichofanyika Ukumbi wa Naliendele uliko katika uwanja wa Ngongo Lindi
Mikoa ya Mtwara na Lindi imeendelea na maandalizi ya maonesho ya wakulima maarufu kama Nanenane yanayotarajiwa kufanyika Kitaifa katika viwanja vya Ngongo vilivyoko Lindi Agost 2017. Akizungumza baada ya kikao cha maandalizi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Naliendele ulioko uwanjani hapo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi amesema taratibu zote za maandalizi zinaenda vizuri.
Wajumbe kutoka mikoa yote miwili wanaonesha moyo hali ambayo inaashiria uwezekano wa maonesho ya mwaka huu kuwa mazuri kuliko yote yaliyowahi kufanyika.
Mheshimiwa Zambi amesema miezi kadhaa nyuma eneo la viwanja hivyo lilikuwa katika hali isiyoridhisha lakini sasa hali ni nzuri na kila kukicha mabadiliko zaidi yanaendelea kuonekana.
Mwandishi wetu ameshuhudua Wakuu wa Wilaya na Wakutrugenzi wa halmashauri za wilaya mbalimbali katika mikoa hii miwili wakikagua maeneo ya halmashauri zao hali ambayo inaashiria uwezekano wa mambo kuwa mazuri zaidi kwa wakati.
Mikoa ya Mtwara na Lindi itakuwa ikiandaa kwa mara ya nne mfululizo maonesho haya katika ngazi ya kitaifa. Aidha katika maonesho ya mwaka jana Mgeni rasmi katika ufungaji wa maoenesho hayo alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
video ya tukio hilo hii HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.