• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

NIMERIDHISHWA NA UBUNIFU WA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MWENGE WA UHURU¬_WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU MHE. PROF JOYCE NDALICHAKO.

Posted on: March 6th, 2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Prof Joyce Ndalichako ameanza ziara ya siku mbili mkoani Mtwara kukagua hatua za maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa uhuru utakaofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Aprili 02, 2023.


Katika kikao cha ndani na kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mtwara, Profesa Ndalichako amesema ongezeko la miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 400 inaashiria nia njema ya Serikali kumkomboa kila Mtanzania wakiwemo wakazi wa kanda ya kusini.


Profesa Ndalichako ameongeza kuwa heshima ya kuzindua Mwenge iliyoipata Mtwara mwaka 2023 imekuja wakati ambapo Serikali ya awamu ya sita imewekeza mabilioni ya fedha kwenye Sekta za Elimu, Afya, Maji, Miundombinu na Umeme hatua ambayo ni faraja kwa Wanamtwara.


Kuhusu Maandalizi ya Uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Waziri Ndalichako amesema kuwa Mkoa wa Mtwara una nafasi kubwa ya kufanya vizuri ikilinganishwa na mikoa mingine iliyotangulia kutokana na muda wa kutosha wa maandalizi.


Baada ya kukagua mazoezi ya halaiki Prof. Ndalichako amewapongeza wakufunzi pamoja na waalimu kwa kutumia muda mfupi kuwajengea uwezo wanafunzi wanaoshiriki katika halaiki hiyo na kuongeza kuwa uwezo waliouonesha mbele  yake unadhihirisha namna Aprili 02 itakavyokuwa na mvuto wa kipekee.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameishukuru Serikali kwa kutoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 kufanikisha maandalizi ya uzinduzi na kuongeza kuwa Serikali ya Mkoa itahakikisha inazisimamia pesa hizo ipasavyo ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.


Aidha Kanali Abbas ameongeza kuwa Serikali ya mkoa inaendelea kuwahamasisha wadau mbalimbali kushiriki kwa namna mbalimbali ikiwemo kuchangia shughuli za maandalizi na kuongeza kuwa tayari baadhi ya wadau wameanza kujitokeza.


Kwa upande wake Waziri Ndalichako ameuagiza Uongozi wa Mkoa wa Mtwara kuangalia namna bora ya kuhamasisha wananchi waweze kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi na kusema kuwa njia hiyo itaongeza hamasa na shamrashamra katika siku ya Uzinduzi.


Katika ziara hiyo Prof.  Ndalichako pia amepata fursa ya kukagua uwanja wa Nangwanda Sijaona utakaotumika siku ya uzinduzi wa mwenge wa uhuru na kusema kuwa anaridhishwa na hatua za mbalimbali za maboresho zinazoendelea.


MWISHO.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA 2022 November 24, 2021
  • Majina ya watumishi wa umma wanaostahili kulipwa madai ya malimbikizo February 09, 2018
  • KUFANYA MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19 August 30, 2021
  • Matokeo ya Kidato cha NNe 2017 January 30, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • IGENI MFANO WA MTWARA KUBORESHA ELIMU – WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA, PROF ADOLF MKENDA.

    March 16, 2023
  • TUONGEZE JITIHADA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA: KANALI AHMED ABBAS AHMED

    March 08, 2023
  • NIMERIDHISHWA NA UBUNIFU WA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MWENGE WA UHURU¬_WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU MHE. PROF JOYCE NDALICHAKO.

    March 06, 2023
  • LETENI MAONI YENU TUTABORESHA MFUMO WA UTOAJI HAKI_JAJI MKUU MSTAAFU OTHMAN CHANDE.

    February 28, 2023
  • Tazama Zote

Video

Wakulima Mtwara wachangamkia kilimo cha Ufuta
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • NBS
  • IKULU
  • UTUMISHI
  • SALARY SLIP
  • e-GA

Kurasa Mashuhuri

  • TAMISEMI
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.