Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Norbert Shee (kushoto) akikabidhi Msaada wa chakula kwa Mratibu wa Sant Egidio Felician Ponsian
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa ametoa Msaada wa chakula cha Krismas kwa wananchi wenye Mahitaji maalumu mkoani Hapa.
Akikabidhi chakula hicho kwa Jumuia ya SANT EGIDIO iliyoandaa tukio la chakula hicho, Mhasibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara Norbert Shee ambaye alikuwa akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa amesema Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameguswa na tukio hilo, hivyo ameamua kutoa mafuta ya Kula, Maharage, Mchele na nyama vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki tano.
Amesema wenye kuhitaji msaada ni wengi hivyo kunahitajika jitihada za pamoja kwa wadau mbalimbali ili kuwafikia wana jamii wote na kwamba Mkuu wa Mkoa alitamani kujumuika pamoja nao lakini kutokana na kuwa nje ya Mkoa kikazi hakuweza kufanya hivyo.
‘Naamini roho ya upendo ndiyo iliyowasukuma Jumuia ya Sant Egidio kuandaa tukio hili. Ni vema jamii zingine nazo zikaiga jambo hili kwani ni jema na linapendeza mbele za Mungu’.
Akipokea msaada huo uliotolewa katika ukumbi wa Kanisa katoliki Mtwara, Mratibu wa Sant Egidio Mkoani Mtwara, Felician Ponsian kwa niaba ya Taasisi nzima ametoa shuklani kwa msaada huo na kwamba ni ishara kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Mkoa mwenyewe wako pamoja na wenye mahitaji maalumu. amesema taasisi hiyo imekuwa ikifanya hivyo kutokana na kutambua uwepo wa mahitaji makubwa ya jamii na hivyo wao wameamua kuchukua jukumu hilo kuwaleta pamoja katika furaha.
Kwa upande wake Naomi saidi Mkazi wa Miembeni Mjini Mtwara ambaye ni mmoja wa washiriki wa chakula hicho amesema anashukuru wanapoona viongozi wao wakiwa karibu nao. Amewata waendelee na moyo huohuo.
Video yake Hii HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.