RC Mtwara akizungumza wakati wa kikao cha Baraza Maalum la Madiwani la kujibu hoja za Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG)
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Halima Dendego amemuagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mtwara Omari Kipanga kumsimaisha kazi Mkuu wa Idara ya Ardhi Katika halmshauri hiyo, Denis Kitali kutokana na kukiuka makubaliano ya idara ya ardhi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa juu ya namna bora ya uendelezaji wa eneo la viwanjwa Msijute kilipo kiwanda cha Saruji cha Dangote.
Akitangaza uamuzi huo katika kikao cha Baraza Maalum la Madiwani la kujibu hoja za Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), mkuu huyo amesema licha ya kusimamishwa kazi, hatua nyingine za kisheria zitafuata dhidi yake.
Mheshimiwa Dendego amesema mpango wa kupima eneo hilo kwa ajili ya viwanda ulifikiwa kwa makubaliano kati ya Ofisi yake na Halmshauri hiyo ambapo mkuu huyo alishiriki kikamilifu tangu mwanzo.
Amesema kilichomshangaza ni Mkuu huyo kuwaeleza madiwani kuwa vipo viwanja 380 ambavyo Halmashauri inampango wa kuviuza ili kuongeza mapato ya halmashauri. Amesema hilo ni suala lisilokubalika na amekuwa akiwasiliana naye kwa maneno na kwa maandishi zaidi ya mara tano akimuelekeza juu ya mpango mzuri wa uendelezaji wa eneo hilo.
Aidha, Mhe. Dendego ameendelea kusisitiza kuwa kama yupo kiongozi yeyote aliyekwisha chukua fedha azirudishe kwani msimamo wake ni huo huo na hautabadilika. Amesema lengo lake ni kuwa na mji wa kisasa wa Mtwara. wenye viwanda vinavyokwenda na mahitaji ya kisasa.
Nao baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo, akiwamo Maupa Abdul na Ramadhan Mfaume wameelekeza lawama zao kwa idara ya ardhi ya halmashauri hiyo kwa kutotimiza wajibu wao kikamilifu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.