Wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara wakifuatilia mijadala
Tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa imebaini mapungufu katika ubora wa barabara zilizojengwa na Wakala wa Barabara Vijijini na mijini (Tarura) katika halmashauri ya wilaya ya Masasi na Manispaa ya Mtwara Mikindani. Tume hiyo aliiunda mapema mwaka huu baada ya kutilia mashakaubora wa baadhi ya barabara katika halmashauri ya manispaa ya Mtwara mikindani. Kufuatia mapungufu hayo Mheshimiwa Byakanwa ameagiza ujenzi huo urudiwe.
Aidha ameagiza Mameneja wa Tarura Katika halmashauri zote kupitia upya orodha ya wakandarasi walioko katika maeneo yao ili kubaini viwango vya utendaji kazi wao.
Byakanwa ameyasema hayo leo katika kikao cha Bodi ya barabara kilichofanyika ukumbi wa Boma mkoa. Amesema halmashauri ambayo ujenzi wake umekuwa na ubora zaidi ni halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu.
“Tunawajibu wa kuhakikisha fedha za serikali zinafanya kama ilivyokusudiwa. Kama kandarasi hafanyi kazi sawaswa hakuna haja ya kuendelea naye”. Amesema Byakanwa.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Mheshimiwa George Mkuchika ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora na Mbunge wa Newala Mjini kimeshauri serikali ijenge daraja katika kijiji cha Kilambo. Kwa sasa eneo hilo hilo linalopakana na Msumbiji likitenganishwa na mto Ruvuma linapitika kupitia kivuko cha MV kilambo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.