Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa Mtwara, Aman Lusake akionesha salfa iliyothibitishwa na TPRI kuwa haifai kwa matumizi
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego ametoa saa 48 kwa wote wanaohusika na tuhuma za safirishaji wa Pembejeo zilizoisha muda wake kutoka ghala la Naliendele kwenda wakulima wilayani Tandahimba warejee kujibu tuhuma zinazowakabili.
Amesema pamoja na kwamba suala hilo amelikabidhi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa, bado anaagiza wote wanaohusika na tuhuma hizo hata kama wako nje ya mkoa warejee ndani ya saa 48.
Agizo hilo amelitoa leo baada ya uchunguzi uliofanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa katika ghala linalotuhumiwa kusafirisha Salfa hiyo kujiridhisha na utata wa ubora wa pembejeo hiyo.
Salfa hiyo inayokisiwa kufikia tani 20 ilisafirishwa kutoka ghala hilo lililoko eneo la Naliendele mkoani Mtwara kuelekea Wialayani Tandahimba na kukamatwa Juni 30 mwaka huu.
Mheshimiwa Dendego amesema ameshatoa maelekezo kwa wakulima wasitumie dawa hiyo na kwamba serikali itaendelea kusimamia kuhakikisha mkulima anapata bidhaa yenye ubora stahili.
Aidha Mheshimiwa Dendego ameeleza kuwa ataunda kikosi kazi kufanya uchunguzi iwapo salfa iliyoenda kwa wakulima ni tani 20 pekee. Uamuzi huo unafuatia taarifa ya wasimamizi wa ghala hilo kwamba walisafirisha tani 20 pekee kati ya tani 75 zilizokuwemo.
Akizungumzia kuhusu tuhuma hizo Mhandisi wa Kilimo Mkoa Amani Lusake amesema Salfa hiyo ilikamatwa mwishoni mwa mwezi wa 6 mwaka huu ikiwa imesafirishwa kwenda Tandahimba na kwamba baada ya taarifa hizo kufikishwa kwa mamlaka ya uchunguzi wa ubora wa salfa hiyo (TPRI) wataalamu hao walitoa taarifa kuwa salfa hiyo imeisha muda wake na kwamba haistahili kwa matumizi.
Kwa upande wake Mkaguzi wa Ndani Bodi ya Korosho Mary Mapunda amesema yeye aliambiwa kuruhusu salfa hiyo kwenda kwa wakulima pasipo kujua iwapo ina ubora stahili. Aidha hata mnunuzi aliyekuja kuichukua alieleza kuwa anaihitaji kwa matumizi ya bustani..
VIdeo ya tukio bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.