• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

RC Mtwara awataka wasanii kujenga chuo cha Sanaa Mtwara

Posted on: November 23rd, 2018

Msanii Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinum akikabidhi fedha taslimu kwa mmoja wa akina mama wakati wa ziara yao ya kundi la Wasafi linalotarajia kutumbuiza kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona kesho Novemba 24, 2018.


Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amewataka wasanii kujenga chuo cha Sanaa mkoani Mtwara. Amesema Mkoa wa Mtwara una vipaji vingi vya sanaa lakini hakuna chuo cha kuweza kuwaandaa kitaaluma.
Mheshimiwa Byakanwa ameyasema hayo leo wakati alipotembelewa na kikundi cha wasanii cha Wasafi ambacho kinatarajia kufanya tamasha la burudani kesho Novemba 24, 2018 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona ulioko Mjini Mtwara.
Amesema sanaa ni ajira, sanaa ni fursa, sanaa ni nafasi ya kujikomboa kimaisha lakini ina muda wake ambao msanii anatakiwa kujiandaa ili wakati huo ukifika awe na njia mbadala ya kuendeleza maisha.
Mtwara kuna waigizaji wengi, kuna wasanii wengi na watu wa Mtwara wanapenda sanaa. lakini kama taifa tuna vyuo vichache sana vinavyoweza kuzalisha wasanii… tunawea kuwa na taasii ambayo tunaweza kuzalisha wasanii wengi na vipaji vingi zaidi. hizo ni fursa ambazo zipo. Mnaweza kuzitumia kwa pesa mnazozipata kwa kipindi hiki. Amesema Byakanwa.
Mheshimiwa Byakanwa amewashukuru wasanii wote wakiongozwa na Msanii Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platinum kwa kuchagua kuja Mtwara. Pia ameshukuru kwa msaada walioutoa kwa makundi mbalibmlai katika jamiii ambao ni pikipiki mbili ambazo wameelekeza ziende kwa shule tatu zinazofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa, milioni tano ambazo zilimetolewa kwa akina mama mia moja ambapo kila mmoja alikabidhiwa shilingi 50,000, sare za shule pea 100 kwa wanafunzi 100 pamoja na madaftari, kalam penseli pamoja na vitabu.
Akizungumzia msada walioutoa, Msanii Diamond Pratinum ameshukuru uongozi wa Mkoa wa Mtwara kwa mapokezi mazuri waliyoyapata. Amesema msaada huo ni kutokana na kuguswa na hali duni ya maisha kwa jamii ya kitanzania.
Amesema msaada huo haujatoka kwa wasafi peke yao bali ni kundi zima la wasanii waliombatana pamoja kuja Mtwara
kwa upande wake Msanii Dudu baya ameshukuru serikali zote zilizotangulia. Amesema yako maendeleo ambayo wengine wanajifanya hawayaoni wakati yako wazi. Ametolea mfano kuwa miaka ya 2005 barabara ya kuja Mtwara ilikuwa ya vumbi ambapo yeye mwenyewe aliwahi kusafiri na kufika Mtwara akiwa amejaa vumbi hadi masikioni, lakini safari hii amesafiri kwa lami tangu Dar es Salaam hadi Mtwara akiwa katika hali yake ya kawaida ya usafi. Amesema hiyo ni hatua kubwa ya maendeleo kwa Tanzania.
Kikundi cha wasafi kinachojumuisha wanamziki na waigizaji maarufu hapa nchini wako Mtwara kwa ajili ya kufanya tamasha maalumu linalojulikana kama wasafi Festival ambalo litafanyika kesho kwenye uwanja wa Nangwanda sijaona kuanzia saa 12 jioni.

Matukio yote katika picha Bonyeza HAPA

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU KARIBU MTWARA

    May 17, 2025
  • JESHI LA POLISI TANZANIA YATUPIA JICHO MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MTWARA

    May 20, 2025
  • MWENGE WA UHURU MASASI

    May 18, 2025
  • NANYUMBU WAANZISHA BIO ZA MWENGE MTWARA

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.