Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego akishiriki ujenzi wa Maabara Wilayani Tandahimba wakati wa ziara yake ya Ukaguzi wa Maabara Februari 2015.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika Halmashauri. Katika ziara hiyo itakayoanza Julai 10 hadi Juni 14 kwa siku Nne kila Wilaya, Mheshimiwa Dendego atatemblea halmashauri zote za Mkoa huu.
Taarifa iliyotolewa jana na Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Evaristy Masuha kwa Vyombo vya Habari, Mheshimiwa Dendego ataaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu kwa siku Nne kuanzia Julai 10 hadi Juali 14. Julai 15 hadi Julai 19 Mheshimiwa Dendego atakuwa Wilaya ya Masasi kabla ya kurudi ofisini kwa siku 5 ili kujiandaa na ziara ya kuelekea Newala.
Pamoja na kuona, kukagua, kuweka mawe ya Msingi, kufanya mikutano ya Hadhara na kupima kwa ujumla utekelezaji wa ilani ya chama Tawala, Mheshimiwa Dendego ataungana na wakurugenzi hao kwa kuchangia vifaa katika baadhi ya hatua za maendeleo zilizoanzwa na wakurugenzi.
Mheshimiwa Dendego ambaye amekuwepo Hapa mkoani kwa Miaka 3 sasa ataambatana na baadhi ya Wakuu wa Idara wa Ofisi yake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.