Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ametoa rai kwa Boodi ya korosho Tanzania kuwasaidia wawekezaji wa ndani ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki yatakayowezesha kuzalisha ajira kwa wananchi.
Kanali Sawala ametoa rai hiyo mapema leo tarehe 06 Januari 2025 alipotembelea moja ya kiwanda cha kubangua korosho kiitwacho Mkemi agrix kinachomilikiwa na mwekezaji mzawa.
“Nimefurahi kuona kiwanda hiki kinazalisha ajira kwa wananchi wetu hususan mabinti. Niwaombe Bodi ya korosho kuwasaidia wawekezeji hawa wa ndani, hii itachochea uanzishwaji wa viwanda vingine vingi vitakavyozalisha ajira kwa wananchi pia serikali itakusanya kodi.” Alieleza Kanali Sawala.
Kwa upande wake mmliki wa kiwanda hiko, Bw. Salum Mkemi ameipongeza serikali kwa namna inavyoipa thamani zao la korosho kwa kuhakikisha korosho inabanguliwa hapa nchini. Aidha amepongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuifanya bandari ya Mtwara isafirishe korosho zote za Mtwara, Lindi na Ruvuma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.