Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 22 Novemba 2024 ameungana na waombolezaji wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Dkt. Batilda Buriani kushiriki shughuli ya kupumzisha mwili wa aliekuwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga marehemu Selemani Sankwa katika makaburi ya Msafa, Mtwara.
Wakati wa uhai wake, Sankwa aliwahi kuajiriwa serikalini kabla ya kuajiriwa na CCM kwa nafasi mbalimbali ikiwemo Katibu wa siasa na Uenezi mkoa wa Mtwara.
Marehemu Sankwa aliezaliwa 19 Oktoba 1982 alifariki tarehe 20 Novemba 2024 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu ya shinikizo la moyo, kisukari na kiharusi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.