Wakala wa nishati vijijini (REA) mapema leo tarehe 20 Agosti 2025 wametambulisha miradi miwili inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania ikiwa na lengo la kuchochea nishati safi ya kupikia pamoja na umeme wa jua mkoani Mtwara.
Meneja Teknolojia za Nishati, Eng. Michael J. Kyessi ameeleza kuwa jumla ya majiko banifu 8794 yatauzwa kwa bei ya ruzuku ya shilingi 11,200/= badala ya 56,000/= kwa mkoa wa Mtwara.
“Tuna mradi wa kupeleka umeme wa mfumo wa jua katika maeneo ya visiwa nchi nzima, kwa mkoa wa Mtwara huduma itatolewa katika kisiwa cha Namponda kilichopo kijiji cha Ruvula, kata ya Msimbati ambapo kaya 28 zitanufaika.” Alieleza Eng. Kyessi
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye amewahakikishia REA pamoja kampuni zitakazotekeleza miradi hiyo ushirikiano wa kutosha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.