Mkuu wa mkoa Mhe. Gelasius Byakanwa (mwenye shati Jeupe) akikagua ujenzi wa mfereji wa maji kutoka Skoya, Nabwaba, Shakur hadi Mtepwezi.
Serikali kupitia mradi wa uendelezaji miji Mkakati (Tanzania Strategic Cities Project) imetoa bilioni 21.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimblai ya maendeleo katika Manispaa ya Mtwara mikindani. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi Wa barabara 4 za mitaa kwa kiwango cha lami, Ujenzi wa maeneo matatu ya kupumzikia (Recreation Center), mfereji mkubwa wa kuondoa maji ya mvua, ujenzi wa soko la kisasa pamoja na kituo cha mabasi eneo la Chipuputa.
Akizungumza leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda amesema fedha hizo zimetolewa kwa mkopo na Benki ya dunia na kwamba ujenzi wa miradi hiyo yote inatarajiwa kukamilika ifikapo oktoba 2019.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutaufanya mji wa mtwara kuwa na muonekano mzuri na kwamba hiyo ndiyo hatua nzuri kuifanya Manispaa kuwa na sifa ya kuwa jiji.
“Naamini baada ya kukamilika miradi hii Mtwara itakuwa sehemu nyingine na pengine inaweza kupata sifa ya kuelekea kuwa jiji”.
Amewataka vijana waliopata nafasi ya kuajiliwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo kuwa waamifu ili kujijengea imani kwa waajili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.