Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ametembelea shule ya Sekondari Dinyecha iliyopo katika Kijiji cha Chikwaya ambayo ipo katika ujenzi kujionea namna shughuli zinavyoendelea na kupata nafasi ya kusalimiana na wananchi pamoja na wakandarasi wa ujenzi huo.
Akiwa shuleni hapo amemuagiza mkandarasi kuongeza kasi ya utendaji kazi kwasababu fedha zipo huku akimtaka mkandarasi huyo afanye kazi mchana na usiku kwani ili amalize ujenzi mapema kabla ya Muhula mpya wa masomo haujaanza ili wakati utakapofika shule hiyo iweze kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha tano mwaka huu.
Aidha Mhe. Kassim Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri Mji Nanyamba kusimamia ujenzi huo ili kusaidia kuongeza hamasa kwa mkandarasi ili aweze kumaliza wakati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.