Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iko katika hatua yamwisho ya ukamilishaji wa ujenzi wa soko la kisasa katika Manispaa ya MtwaraMikindani.
Picha na maelezo zaidi HAPA
Soko hili linatarajiwa kugharimu shilingibilioni 4.8 ambazo ni mkopo toka Benki ya Dunia kupitia mradi wa ujenzi nauendelezaji wa miji ya Kimkakati Tanzania (TSCP) na linatarajiwa kukamilikaMwezi Mei, 2020.
Licha ya kuondoa changamoto nyingi zawafanyabiashara na wananchi wa Mtwara kwa ujumla, soko hili linatarajiwakuupamba mji wa Mtwara kutokana na muonekano mzuri ambao unaleta hadhi kwaManispaa ambayo inaendelea na miradi mingine yenye sifa hiyo. Miradi hiyo nipamoja na mradi wa bustani za mapumziko, (recreation Centres), Mifereji yakuondoa maji ya mvua, barabara za lami na mingine mingi ambayo yoteinatekelezwa kupitia mkopo huo.
Soko hili ambalo halijatambulishwa jinalake rasmi limejengwa katika mtaa wa Chuno, ambao una barabara nzuri inayopitikakipindi chote cha masika na kiangazi huku ikiwa na taa za kisasa ambazozinatumia umeme wa jua kuwahakikishia watumiaji wake usalama kwa muda wote. Piani barabara maarufu ambayo inaelekea maeneo mbalimbali ya fukwe maarufu kamavile Makonde, Kianga na Msangamkuu. Pia hotel Maarufu ya Naff Beach.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmandaanasema soko hilo litakuwa na uwezo wa kuhudumia makundi mbalimbali ya kijamii.Litakuwa na sehemu za kuweka migahawa, Ofisi na huduma nyingine nyingi nalimejengwa kwa namna rafiki kwa watu wa aina zote. Aidha, gharama za kupangakatika jengo hilo zitakuwa rafiki ili kuwezesha wananchi wa wilaya ya Mtwarakunufaika na huduma hiyo.
Kwa upande wao wananchi wa Manispaa yaMtwara Mikindani wameipongeza serikali kwa ujenzi wa soko hilo na kwambalitaongeza mapato na ubora wa bidhaa ambao umekuwa ukipotea kutokana nachangamoto ya uhifadhi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.