(TCCIA) Mkoani Mtwara imetoa ushauri kwa Serikali kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara mkoani humo ili kuboresha mazingira ya biashara ndani ya Mkoa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika hivi karibuni katika Mikoa kumi nchini ikiwemo Mkoa wa Mtwara na Shirika lisilo la Kiserikali la Kibelgiji (Trias Tanzania) yenye Makao makuu yake Jijini Arusha kwa kushirikiana na TCCIA umeonyesha pengo kubwa la umiliki wa biashara kwa makundi ya Jinsia mbalimbali ikiwemo wanawake na Vijana kwani mazingira ya biashara yamekuwa siyo mazuri kutokana na elimu ndogo ikilinganishwa na makundi ya umiliki wa biashara wa pamoja ambapo kwa mkoa kumefanyika tafiti 280.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Tanzania TCCIA Mkoani Mtwara Athumani Akida ametoa mapendekezo ya maboresho ya Sekta ya biashara nchini wakati wa Baraza Maalum la Biashara Mkoa wa Mtwara lililofanyika ukumbi wa BOT Mjini Mtwara na kukutanisha wajumbe kutoka Taasisi mbalimbali lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya biashara ndani ya Mkoa wa Mtwara.
Utafiti umefanyika katika Mikoa kumi ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Dodoma, Kigoma, Mara, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Shinyanga pamoja Songwe lengo kubwa likiwa ni kuboresha mazingira ya biashara kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi.
Alisema kuwa, ili biashara ziweze kwenda vizuri ni lazima kuwe na elimu ya kutosha kwa wafanyabiashara hivyo Taasisi za Serikali zinazohusika moja kwa moja na wafanyabiashara ziweke utaratibu wa kutoa elimu juu ya namna ambavyo wafanyabiashara hao wanatakiwa kufanya katika uendeshaji wa biashara zao.
“Elimu ni nzuri sana na huu ni mwanzo nzuri na tunahitaji elimu iwe endelevu kwani itasaidia mfanyabiashara kujua nini cha kufanya na nini anatakiwa kuboresha kwenye biashara yake ili aweze kuendesha biashara katika malengo yanayotakiwa”,Alisema Akida
Meneja wa mradi huo wa BULDING BRIDGES TRIAS David Attar alisema kuwa katika utafiti huo wameona umiliki wa biashara kwa wanawake na vijana Mkoani Mtwara uko chini, namna wanavyopata huduma kutoka katika Taasisi mbalimbali, uaminifu, na utayari wa kutoa huduma kwa wafanyabiashara hao, kufanyia kazi maoni yanayotolewa na wafanyabiashara hao, ushirikishwaji wa wafanyabiashara wadogo. Pamoja na mambo hayo yote kubwa ambalo wameona ni mazingira ya biashara kutokuwa mazuri.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho akiwemo Sophia Kitale alisema kuwa, katika suala la ushirikishwaji kwenye masuala ya fursa mkoani humo wamekuwa hawapati kwa wakati kwani wangekuwa wanapata taarifa za fursa hizo kwa wakati ni matumaini yake biashara zingeweza kwenda vizuri.
Mwenyekiti wa kikao Ndg. Abdallah Malela ambaye pia ni Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara amesema kuwa kama Serikali itahakikisha inasimamia na kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiashara na pia kuwapa elimu ya kutosha kwani lengo ni kuhakikisha mazingira ya biashara yanakuwa mazuri kwa Mkoa wa Mtwara.
Pichani; Baadhi ya washiriki kwenye kikao cha Baraza la Biashara kilichofanyika ukumbi wa BOT Mtwara Agosti 18 2021
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.