Mkoa wa Mtwara Umepokea jumla ya vitabu 11,812 kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET). Vitabu hivyo vya kiada vimekabidhiwa jana Januari 29, 2019 kisha kusambazwa wilaya zote za Mkoa wa Mtwara. Vitabu hivyo vinalenga kuondoa changamoto ya uhaba wa Vitabu katika shule zote za Msingi na sekondari kwa mkoa wa Mtwara ikiwa ni utekelezaji wa mikakati ya uboreshaji wa Elimu nchini unaoenda sambamba na sera ya Elimu Bila malipo.
Akizungumzia tukio hilo Mwakilishi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Bi. Joyce Shuma. Amesema vitabu vilivyoletwa mkoa wa Mtwara ni pamoja na vile vitakavyotumiwa na wanafunzi wa Kidato cha kwanza na cha pili kwa masomo ya Historia na Jiografia, na Kidato cha Sita kwa masomo ya Sayansi (Kemia, Fizikia, Biolojia na Hisabati).
Aidha Idara ya Elimu Msingi imepokea Vitabu vya kujifunzia kwa wanafunzi wa darasa la sita na vitabu vya kufundishia vya walimu katika masomo ya Kiswahili, Hisabati, Sayansi na Teknolojia, Maarifa ya Jamii, Stadi za kazi, Uraia na Maadili pamoja na somo la kingereza.
Akizungumza wakati wa kupokea Vitabu hivyo Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mtwara Salum Masalanga ameishukuru Serikali kwa kuleta vitabu hivyo na kwamba vitasaidia kuondoa changamaoto ya uhaba wa Vitabu katika shule zote hivyo ufundishaji utakuwa rahisi Zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.