Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ameongoza zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linaloratibiwa na Tume huru ya Uchaguzi lililoanza mapema leo tarehe 28 Januari 2025 lenye lengo la kuandikisha wapiga kura wapya na kuboresha taarifa za wapiga kura walioandikishwa kwaajili ya Uchaguzi mkuu wa 2025.
“Mwaka 2020 sikuwa Mtwara, saizi nipo Mtwara hivyo imenibidi nije nirekebishe taarifa zangu na nimeshapata kitambulisho. Tutambue muda tulio nao ni juma moja hivyo nitoe wito kwa wana Mtwara wenzangu kujitokeza kuboresha taarifa, kwa wale ambao wametimiza miaka 18 au watatimiza siku ya kupiga kura na wale waliopoteza kadi wote wajitokeze katika zoezi hili.” Alieleza Kanali Sawala
Akieleza hali ya usalama kwenye mipaka na dhana ya wasio watanzania kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura, Kanali Sawala alisema, Tume huru ya Uchaguzi imejipanga vizuri, imetoa mafunzo kwa watendaji wake kuhakikisha ni watanzania pekee ndio watakaopata kadi za kupiga kura.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa mkoa wa Mtwara litatamatika tarehe 03 Februari 2025.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.