Katibu Mkuu Or-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe ametolea ufafanuzi wa namna ulivyofanyika uchaguzi wa Wanafunzi kujiunga kidato Cha tano na vyuo vya Kati ili kuondoa sintofahamu iliyoletwa na wachache wasiyoitakia mema Nchi.Profesa Shemdoe amesema kuwa kabla ya kuchaguliwa watahiniwa huwa wanajaza fomu maalumu zinazowataka kupendekeza Tahsusi tano anazopenda kuendelea kusoma endapo atafaulu kidato Cha nne.Ameendelea kusema kuwa wakati wa kuwachagua kunakuwa na ushindani kulingana na alama alizopata Mwanafunzi na nafasi zilizopo katika Shule na Tahsusi husika hivyo chaguo la kwanza lisipofanikiwa zinaangaliwa zingine.Kwahiyo hakuna Mwanafunzi aliyechaguliwa katika Tahsusi ambayo hakuipendekeza kwenye fomu hata mfumo umethibitisha hivyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.