Kifaa cha Umeme Tayari (UMETA)
Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Medard Kalemani amewataka watanzania kuchangumkia fursa ya kuunganishiwa umeme kwa kutumia kifaa kinachojulikana kama Umeme Tayari (UMETA). Amesema kifaa hicho kinamuepusha mtumiaji na gharama za kufanya ‘wiring’ na hivyo kupunguza gharama za kuingiza umeme kwenye nyumba.
Waziri ameyasema hayo jana katika maeneo tofauti alipokuwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mtwara.
“Serikali imeamua kuwapungumzia gharama wananchi kwani ukishaweka hicho chombo hulazimiki tena kufanya ‘wiring’ ...Kwa vile hicho kifaa kinafaa kwa matumizi yote isipokuwa viwanda tunawashauri wnanchi wavitumie. Pia tunashauri vifaa hivi vitumike kwenye taasisi za Umma kama ofisi za vijiji vituo vya afya, vituo vya polisi, zahanati na maeneo mengine ambayo kimsingi si lazima sana ufanye wiring.” Amesema Waziri.
Amesisitiza kwamba serikali imewataka wakandarasi wahakikishe wanavitoa bure kwa wateja wa kwanza mia moja hadi mia mbili hamsini. Baada ya hapo vinakuwa vinauzwa kwa bei ya serikali ambayo ni shilingi 36,000.
kwa kuanzia Mheshimiwa waziri amegawa vifaa 250 kwa kila jimbo alilotembelea mkoani hapa ikiwemo Lulindi, Nanyamba na Newala.
Pamoja na punguza hilo amesema serikali bado inaendelea na punguza la kuingiza umeme kupitia mradi wa REA ambapo gharama yake ni shilingi elfu 27 tu.
Video yake hii HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.