Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Gasper Byakanwa ameahidi kutoa huduma bila kubagua kundi lolote katika jamii. Mheshimiwa Byakanwa aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huu Oktoba mwaka huu amesema Serikali ya awamu ya Tano anayoitumikia imejikita kuhudumia watu bila kuangalia itikadi zao, hivyo yeye kwa nafasi yake atahakikisha anawahudumia watu wote bila kuangalia itikadi zao kwani misingi ya Umoja wa Watanzania hauendani na itikadi za utengano wa imani yoyote bali Tanzania ni ya wote na umoja ndio msingi wa watanzania.
Mheshimiwa Byakanwa ameyasema hayo wiki hii wakati akizungumza na wazee maarufu pamoja na viongozi wa Dini kwenye kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Boma Mkoa.
Amesema anatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Mtwara ikiwemo suala la elimu hivyo amemuagiza Katibu Tawala Mkoa aitishe kikao cha wadau wa Elimu ili kujadili kwa pamoja changamoto hizo.
Kwa upande wa uhaba wa magunia ya kuuzia korosho amewaagiza Bodi ya Korosho kuhakikisha wanasambaza kwa kila mkulima ili isitokee yeyote akakossa gunia. Aidha msimamo wa kusafirisha korosho ghafi kwenda nje ya nchi kupitia bandari ya Mtwara uko palepale.
Kwa Dondoo na mengi yaliyojiri katika kikao hicho soma hapa.
*YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA MKUU WA MKOA WA MTWARA MHE: GELASIUS G. BYAKANWA NA WAZEE MAARUFU PAMOJA NA VIONGOZI WA DINI JANA NOVEMBA 21, 2017 UKUMBI WA BOMA MKOA.*
-Amewashukuru wazee na viongozi kwa mahudhurio makubwa kwani imempa faraja kuwa wenyeji wapo na wamempokea vema
-Ameahidi kukutana na viongozi hao kila baada ya miezi sita kujadililiana masuala mbalimbali na kupeana mrejesho wa yale yote yaliyojadiliwa kwenye kikao kilichopita
-Amewataka wataalamu kufanyia kazi ushauri uliotolewa na wazee pamoja na viongozi wa DINI na kutoa majibu ya kisayansi
-Ametoa agizo kwa benki zote kutenga dirisha maalumu la kuhudumia wazee, akina mama wajawazito na watu wenye mahitaji maalumu
-Serikali ya awamu ya tano imejikita kuhudumia watu bila kuangalia itikadi zao, "Naahidi nitahudumia watu wote bila kuangalia itikadi zao nikiamini misingi ya Umoja wetu hayaendani na itikadi hizo kwani Tanzania ni yetu, Umoja ni wetu"
-Wananchi muna jukumu la kutoa taarifa kwa watu mnaowashuku kwenye maeneo yenu
-Naagiza Wakuu wa Wilaya, Watendaji wa Mitaa/vitongoji kuwa na orodha ya wakazi kwenye maeneo yenu
-Amewataka wakurugenzi kuwasimamia wenyeviti wa mitaa/kitongoji kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe ameorodhesha Wananchi wanaoishi kwenye eneo lake wanaoanzia umri wa miaka 18 na kuendelea na NDANI ya miezi 3 zoezi liwe limekamilika
-Amemuagiza Katibu Tawala Mkoa aitishe kikao cha wadau wa Elimu ili kujadili kwa pamoja changamoto za elimu
-"Changamoto za watoto wa kike kupata mimba shuleni nazitambua, kwenye kikao cha wadau tutaona njia bora ya kuboresha Elimu"
-Ameagiza bodi ya korosho wahakikishe magunia yanasambazwa kwenye maeneo yote
-Atahakikisha kila mkulima anapata gunia litakalobeba korosho na si kitu kingine
-Serikali ya Mkoa tumeamua na tumesisitiza wafanyabiashara wa korosho kutumia Bandari ya Mtwara
-Nimepata taarifa kutoka kwa Meneja wa Bandari Mtwara kuwa hadi wiki iliyopita Bandari imekusanya Shilingi Bilioni 24
-Zao la korosho limetoa ajira nyingi kwa wananchi wa Mtwara
-Ni utaratibu wa Serikali na maelekezo kuwa Malipo yote ya wakulima wa korosho yatapitia Benki
-Amewaomba viongozi wa DINI na wazee waendelee kutoa Elimu kwa Wananchi wetu wafungue akaunti Benki.
-Amewasisitiza wananchi kutoa Pesa kidogo kidogo na wawe na utamaduni wa kuweka akiba
-Amewataka wakulima wanapoenda kutoa fedha Benki watoe kulingana na mahitaji yao,ukibeba fedha nyingi unahatarisha maisha yako
-Tunapofurahia bei nzuri ya korosho nendeni mkakate Bima ya Afya
-Wakurugenzi muna jukumu la kuniandalia baada ya msimu kuisha wananchi wangapi wamejiunga kwenye Mfumo wa Bima ya Afya
-Amewataka wakulima kusomesha watoto wako kutoka na na fedha za korosho
-Mkurugenzi wa Manispaa sitaki kuona watu waancheza pool muda wa kazi wala pombe kuuzwa muda wa kazi
-Nitakaa na bodi ya Timu Ndanda na wadau wanaotaka kuiendeleza Timu kwa pamoja tujadili Namba ya kuiendesha timu hiyo ili iendelee kubaki kwenye ligi juu na vijana wetu pia wasikose ajira
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.