Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa akiangalia baadhi ya mifugo katika mabanda ya maonesho ya wakulima Nanenane kanda ya kusini yaliyofanyika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi
Wadau wa maonesho ya wakulima (Nanenane) wamezitaka taasisi zilizo na mabanda katika viwanja vya ngongo yanakofanyika maonesho hayo kwa Kanda ya Kusini kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kuwezesha mabanda hayo kufanya kazi kwa kipindi cha mwaka mzima.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa shughuli zinazofanyika katika viwanja hivyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa, amesema kufanya hivyo kutafanya eneo hilo liwe hai kwa kipindi cha mwaka mzima na hivyo kuzisaidia halmashauri na taasisi husika kupunguza gharama za usafi wa mazingira kipindi maonensho yanapokaribia pamoja na kuwa chanzo kizuri cha mapato.
“ Jambo ninalolitaka kwa halmashauri zetu ni kuyafanya maeneo haya kutumika kwa kipindi chote cha mwaka. Hii ni changamoto ambayo lazima tupate majibu yake kwa sababu rasilimali zote tulizoziweka hapa zimekuwa zinaisha mara baada ya maonesho ya Nanenane. Tunachokitaka sasa wawepo kwa Muda mrefu.”
Aidha amezishukuru taasisi ambazo zimeanza utaratibu huo ikiwemo halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Jeshi la Kujenga Taifa, Magereza na taasisi zingine zote ambazo ziko katika hatua mbalimbali ya kuhakikisha mabanda yao yanakuwa hai katika viwanja hivyo wakati wote.
Naye Mgeni Rasmi wa maonesho hayo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba ameongeza kuwa miundombinu iliyoandaliwa kwa ajili ya maoensho haya ngazi ya kanda ya kusini yaendelezwe. Amesema serikali iliwahi kuweka mazingira kwa ajili ya wananchi kujifunza kilimo katika ngazi ya kata hivyo viongozi wanajukumu la kuhakikisha miundombinu hiyo inaendelezwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.