Mkuu wa Wilaya ya Newala Mheshimiwa Aziza Mangosongo ameagiza kukatwa mishahara wahandishi wa ujenzi wa Halmashauri ya Mji wa Newala kwa kosa la kushindwa kusimamia ipasavyo mradi wa ujenzi wa bwalo la kulia chakula wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiuta kulikosababisha sakafu kuwa na ufa na hivyo kuilazimu halmashauri kuivunja na kuweka nyingine kwa gharama ya shilingi milioni moja na laki nane.
Mheshimiwa Mangosongo ameyasema hayo wakati wa ziara ya Mwenge wa Uhuru uliotembelea shule hiyo kwa lengo la kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Bwalo hilo. Amesema kuwa alitembelea shule hiyo mapema mwaka huu na kubaini ubovu wa sakafu hiyo ndipo akaagiza ivunjwe na kujengwa upya. Hata hivyo ameshangazwa na kutokuta mabaki ya sakafu iliyovunjwa baada ya kuelezwa na Mkuu wa Shule hiyo kuwa aliyafukia ili kusafisha mazingira. Amesema hilo haliwezekani, hakuna Mtumishi anayevumiliwa kwa kutotimiza wajibu wake.
kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Charles Kabeho amesema ujenzi huo ambao unasimamiwa na Kamati ya Shule umekosa usimamizi wa kutosha wa wahandisi hali ambayo imesababisha kasoro hizo. Amewataka wabadilike ili kutimiza wajibu waoa kama watumishi wa umma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.