Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mzee Mkongea Ali akikagua bidhaa za wajasiliamali.
Halmashauri ya Mji wa Masasi imetoa mkopo wenye thamani ya shilingi 79,500,000. sawa na asilimia 101.19 ya pesa iliyotakiwa kukopeshwa vikundi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.
Akizungumza leo wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Sospeter Nachunga amesema fedha hizo zimetolewa kwa vikundi 16 vyenye jumla ya wajasiliamali 155.
Amesema hayo ni mafanikio makubwa kwa halmashauri ukilinganisha na hali ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
“Naishukuru sana serikali ya awamu ya tano imetuwezesha kusimamimia vizuri mapato jambo ambalo limeongeza uwezo wa wa halmashauri kusaidia jamii. Tunaamini mwaka huu tutakuwa na mafanikio makubwa zaidi ya haya”.
Nachunga ambaye pia ni diwani wa kata ya Napupa amewataka vijana, akina mama na walemavu kuhakikisha wanajiunga katika vikundi ili iwe rahisi kukopesheka.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Mzee Mkongea Ali amepongeza hatua hiyo na kuwataka wajasiliamali walionufaika na mikopo hiyo kuhakikisha wanatumia fursa hiyo kujiinua kiuchumi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.