• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

Wajerumani kujenga kiwanda cha Mbolea Mtwara. kitakuwa kikubwa kuliko vyote Afrika

Posted on: May 5th, 2018

Mwakilishi wa kampuni ya HELM A.G katika bara la Africa, Mohamed Maatouk.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mheshimiwa Balozi Dkt. Augustine Phillip Mahiga amesema moja ya uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na wajerumani hapa nchini ni ujenzi wa kiwanda cha Mbolea mjini Mtwara. Mheshimiwa Mahiga ameyasema hayo juzi mara baada ya kikao kifupi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani Mhe. Heiko Maas aliyekuwa katika ziara ya siku mbili hapa nchini. Amesema kiwanda hicho kitakuwa kikubwa kuliko vyote Afrika.

 ‘Tumezungumzia eneo la uwekezaji, uwekezaji katika sekta mbalimbali za viwanda. viwanda katika kutengeneza ajira, viwanda kutuwezesha sisi kufikia lengo letu la kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 na Ujerumani kama nchi yenye nguvu, na ambayo ina uwezo mkubwa kuliko nchi zote za magharibi mwa Ulaya inaweza kuwa  Mwekezaji mkubwa katika nchi yetu.

 Tayari sasa hivi tunazungumza uwekezaji wa kiwanda ambacho kitakuwa kikubwa kuliko vyote Afrika, kiwanda cha kutengeneza mbolea huko Mtwara. kiwanda ambacho kitasaidia wakulima na kitatengeneza ajira kwa watanzania’ Amesema Balozi Mahiga.

Mheshimiwa Mahiga ambaye video ya dakika moja ya maelezo yake inapatikana kwa kubonyeza HAPA amesema uhusiano wa Tanzania na Ujerumani ni wa kihistoria na ndiyo maana Waziri huyo ambaye amepewa nafasi hiyo hivi majuzi ameamua kufanya ziara yake ya kwanza Barani Afrika hapa nchini. Amesisitiza kuwa kutokana na uwezo mkubwa wa uchumi wa taifa la Ujerumani wanauwezo wa kuwa  wawekezaji wakubwa katika nchi yetu.


Wajerumani kujenga kiwanda kikubwa cha mbolea Mtwara 

Majadiliano ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya HELM yenye makao yake Ujerumani yalianza miaka kadhaa huko nyuma. Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding) kati ya Kampuni hiyo na Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mtwara (RCC) kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Mtwara ilisainiwa Julai 21, 2014.

Matarajio makubwa ya wananchi wa Mtwara ni kuwa kujengwa kwa kiwanda hiki kutawezesha ndoto ya uongozi wa Mkoa wa Mtwara kuhakikisha ifikapo mwaka 2035 Mtwara kinakuwa kituo muhimu cha uwekezaji na kitovu cha huduma na shughuli muhimu za usafiri na usafirishaji katika ukanda wa mikoa ya kusini mwa Tanzania hususani mikoa ya Lindi, Mtwara Ruvuma na Njombe na ukanda wa maendeleo wa Mtwara ambao unahusisha nchi za Tanzania, Msumbiji, Malawi, Zambia na Afrika ya kusini.

Pia kuifanya Mtwara kuwa Jiji lenye ustawi wa maisha shindani na majiji yaliyo kwenye ukanda wa bahari ya hindi, mashariki na kusini mwa Afrika.


Picha za tukio na maelezo zaidi Bonyeza HAPA

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC SAWALA "ACHENI KUFANYA KAZI KWA MAZOEA"

    June 21, 2025
  • MTWARA MWENYEJI WA MAFUNZO YA KOROSHO BARA LA AFRIKA.

    June 23, 2025
  • NHIF YAFANYA MAZUMGUMZO NA RC SAWALA

    June 23, 2025
  • RC SAWALA AAGIZA VYAMA VYA USHIRIKA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WAKULIMA

    June 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.