Serikali imeahidi kuwalipa wakulima wote wa korosho ambao hadi sasa hawajalipwa malipo yao ya msimu wa 2018/2019.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mhe. Selemani Mzee wakati anazindua maonesho ya NANENANE kwa kanda ya Kusini, yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo, Manispaa ya Lindi.
Seleman ambaye alikuwa Mgeni Rasmi kwa niaba ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jaffo, alisema serikali imedhamiria kuwalipa wakulima wote Ambapo
zoezi la malipo linaendelea.
Mzee amesema wakulima hao pamoja na wale ambao walinunua zao hilo nje ya mfumo rasimi (kangomba) ambao wamepeleka barua za kukiri kununua nje ya mfumo rasmi na wameomba radhi na watalipwa.
'' Walionunua kwa kangomba na waliotii agizo la mheshimiwa Rais kuwa wakiri na waombe msamaha watalipwa kama alivyoahidi. Kwa bahati nzuri wamejitokeza, wamekiri na wameomba msamaha na barua zao tumepokea,'' Amesisitiza Mzee.
Aidha, amekipongeza kituo cha uwekezaji nchini kwa kuandaa kongamano lililosababisha kampuni 14 na washiriki 300 kushiriki kujadili mambo mbalimbali yanayohusu zao hilo.
Kufuatia hali hiyo, Mkuu huyo wa wilaya ya Masasi, kwaniaba ya waziri wa TAMISEMI amewaomba wakulima waongeze uzalishaji katika msimu huu wa 2019/2020. Kwani changamoto za msimu uliopita zimefanyiwa kazi.
Alisisitiza kwamba serikali inatambua umuhimu wa kilimo na wakulima katika uchangiaji wa uchumi wa nchi. Hivyo kwakuzingatia ukweli huo inabeba dhamana ya kuaandaa maonesho hayo kila mwaka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.