• Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

Walimu wa sekondari Mtwara kuhamishiwa Msingi

Posted on: December 21st, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amemuagiza Katibu Tawala Mkoa, Alfred Luanda kuangalia uwezekano wa kuwahamisha walimu wa sekondari ili wafundishe shule za Msingi. Mheshimiwa Byakanwa ametoa agizo hilo wakati wa kikao wa wadau wa Elimu mkoani Mtwara kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara Kawaida.

Amesema haiwezekani mkoa ukakaa kusubiri Wizara ilete walimu wakati walimu wapo. Kinachotakiwa ni kufuata utaratibu na kuangalia walio na sifa za kufundisha shule za Msingi waende bila kuathili mishara yao.

Ametoa agizo hilo kufuatia taarifa ya Afisa Elimu Mkoa Fatuma Kilimia ambayo ilionesha ziada ya walimu 608 wa masomo ya sanaa kwa shule za sekondari Mkoani hapa wakati shule za Msingi Mkoani hapa zikiwa na upungufu wa Walimu 2,836.

Katika taarifa hiyo Kilimia alieleza kuwa mahitaji ya walimu wa masomo ya sanaa kwa shule za sekondari Mkoani Mtwara ni 1490 waliopo 2098 hivyo kufanya ziada ya walimu 608.

Wakichangia katika kikao hicho kilichokusudia kuangazia changamoto za elimu kwa mkoa wa Mtwara wadau wameitaka serikali kuhakikisha inapambana na masuala mbalimbali yanayozuia maendeleo ya elimu.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Nanyamba Mheshimiwa Abdalah Chikota ameitaka serikali ihakikishe inafuatilia mwenendo wa elimu kuanzia ngazi ya shule ili kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa nafasi yake na wanaobainika kutotimiza wajibu wao wawajibishwe. Pia ameitaka serikali kuhakikisha mfuko wa elimu kwa kila halmashauri unasimamiwa ili utumike kwa lengo lililokusudiwa.

Aidha Mkuu wa Shule ya sekondari Mitengo Mwalimu Amina Bakari ameitaka serikali iweke viwango ambavyo kila atakayeshindwa kuvifikia atawajibishwa.

Akiridhia wazo hilo Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ameagiza kila shule kuhakikisha zinakamilisha mtaala wa darasa husika mwezi wa sita wa kila mwaka ili muda unaobaki utumike kufanya majaribio na marudio ya vipengele mbalimbali ndani ya masomo husika.

Mkoa wa Mtwara umekuwa haufanyi vizuri katika mitihani mbalimbalia ya kitaifa hali ambayo inamfanya Mkuu wa Mkoa Mhe. Byakanwa aliyechaguliwa kuongoza mkoa huu hivi karibuni kuitisha kikao hicho chenye lengo la kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo. Katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana mkoa ulishika nafasi ya 22 kati ya mikoa 26.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MWENGE WA UHURU KARIBU MTWARA

    May 17, 2025
  • JESHI LA POLISI TANZANIA YATUPIA JICHO MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA MTWARA

    May 20, 2025
  • MWENGE WA UHURU MASASI

    May 18, 2025
  • NANYUMBU WAANZISHA BIO ZA MWENGE MTWARA

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.